Mohammed Morsi: Rais wa zamani wa misri afariki dunia

Rais wa zamani wa Misri Mohammed Mosri amefariki dunia leo baada ya kujibu mashtaka katika Korti Moja jijini Cairo.

Morsi aliyekua rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini humo mwaka wa 2012 alitimuliwa mamlakani na jeshi la nchi hiyo mnamo mwaka wa 2013 na kutiwa mbaroni mpaka leo hii alipofariki.

Runinga ya serikali ilitoa habari kwamba Morsi alifariki kutokana na mshtuko wa moyo. Morsi aliingia madarakani kama kiongozi wa kundi la Muslim brotherhood ambalo kwa sasa linahusishwa na vitendo vya kigaidi.

Kifo chake kimeibua hisia tofauti huku wengi ikiwemo makundi ya haki za kibinadamu yakitaka uchunguzi zaidi kufanyika kuhusiana na kifo chake morsi. Kundi la Muslim brotherhood kwa upande wao walitaja kifo chake kama mauaji ya hali ya juu, wakipinga habari kuwa alifariki kutokana na mshtuko wa moyo.

Katika mwaka huo mmoja Morsi alipokua madarakani, alikumbwa na madai ya kuanzisha kundi la kigaidi la kiislamu mbali na kuendesha uchumi wa nchi hiyo vibovu. Maandamo makubwa jijini cairo yalielekeza kubanduliwa kwake madarakani huku wafuasi wake wengi wakikamatwa na kutiwa mbaroni katika miaka iliyofwata.

Advertisements

Bilioni mbili bandia zanaswa benki ya Barclays

Mkuu wa Kitengo cha upelelezi nchini George Kinoti amethibitisha habari za kunaswa kwa shilingi bilioni mbili zilizowekwa katika benki ya Barclays, tawi la Queenway jijini Nairobi.

Fedha hizo zilikua zimewekwa katika kuba moja katika benki hiyo na mteja aliyekamatwa asubuhi ya jumanne 19 akiwa katika ziara ya kukagua mali yake.

Kisa hiki kimetokea muda usio mrefu tu baada ya sakata sawia kutokea eneo la Ruiru ambapo polisi walinasa washukiwa watatu kuwafikisha kortini baada ya kupatikana na bilioni thelathini na mbili noti bandia.

 

Ingwe yapata kocha mrwanda sasa

Klabu ya AFC Leopards imetangaza kuingia kwa kocha mpya Andre Casa Mbungo ambaye ana asili ya kirwanda.

Hii ni baada ya kocha wa kitambo Marko Vasiljevic kuaga miamba hao wa soka nchini siku ya Jumatatu.

Marko amewaaga wana ingwe baada ya miezi miwili usukani mwa klabu hiyo, alisimamia mechi 10 huku akipata ushindi mara mbili tu. Alijiuzulu baada ya kupokea kichapo mikononi mwa Bandari.

Mbungo atakua kocha wa tatu kuifunza timu hiyo ya AFC msimu huu huku wakijaribu kutafuta matokeo bora ligi kuu nchini.